top of page
Writer's pictureBranice Nafula

Marioo Tz ,The God Son: Kollabo, Ladha, Ubora



Toto Bad almaarufu kama Marioo ametusogeza karibu kufuatilia safari ya uzinduzi wa albamu yake mpya, mzigo uko tayari kwa wasikilizaji, wapenzi na mashabiki wa muziki mzuri kuisikiliza.

 

Albamu ameipa jina la The God Son, na humo ndani tayari tumeonjeshwa hit kadhaa ambazo tayari zilishatoka na mtaani zimepokelewa vizuri ikiwemo “Unanchekesha”, “2025” na zingine. Ngoma hizo zimesadifu ladha na ubora uliopo kwenye albamu ambayo inazinduliwa leo kwa wadau wa muziki na itakuwa mtaani tarehe 29 Novemba 2024.

 

Marioo kupitia chapisho lake kwenye ukurasa wake wa Instagram ametukaribisha kujua unyama wa kuutegemea kwenye albamu yake. Humo ndani ameshirikisha wakali kutoka Afrika Magharibi ambao ni kama Patoranking wa Nigeria na King Promise kutoka Ghana. Kutoka Afrika Mashariki, Marioo amewashirikisha Bien kutoka Kenya, Kenny Sol na Element Eleeh kutoka Rwanda, na Joshua Baraka kutoka Uganda.

 

Kutoka kiwanda cha burudani cha Tanzania, Marioo kawashirikisha ‘heavy weights’ kama Ali Kiba, Aslay na Harmonize ambao wote kwa nafasi zao ni wakali wa uimbaji lakini pia wana vitu vyao adimu ambavyo kwa uhakika kollabo zao zinatazamiwa kuwa moto wa kuotea mbali.

 

Marioo pia ametutonya uwepo wa msanii ambaye katika label yake ya Bad Nation ambaye nae amepata nafasi ya kufanya wimbo na Marioo, jamaa anaitwa Stans anajulikana kama msanii chipukizi na tunategemea kusikia uwezo wake kupitia kollabo yao.

 

Ubora wa albamu nzima unatazamiwa kuwa hali ya juu kutokana na uwepo wa watayaarishaji wa muziki tofauti, ambao wanajulikana kwa kazi zao  ambazo wameshafanya na Marioo na wasanii wengine. Toto Bad amedokeza kuwa aina za muziki zilizotawala ni Bongo Flava lakini pia na Afrobeats ambayo ni maarufu zaidi kwa nchi kama Nigeria.

 

Tukio la usikilizaji wa albamu ya The God Son linafanyika leo tarehe 28 Novemba 2024, pale Tips Coco Beach. Wadau wa muziki ikiwemo  wanahabari, watangazaji wa muziki, watayaarishaji na watu wanaofahamika wataungana na Marioo kusikilza albamu yake ambayo itakuwa mtaani tarehe 29 Novemba yaani kesho.

 

Mashabiki na wapenzi wa muziki mzuri wameonesha shauku kubwa kutaka kusikiliza kazi ya fundi wa Bongo Flava namna ambavyo ameua humo ndani. Share hapo chini kwenye comment kollabo gani unatamani sana kuisikia kati ya wasanii wote aliowashirikisha.

 

 

4 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page