top of page
Writer's pictureBranice Nafula

5 Za Kwenye Msanii Bora Wa Hip Hop Ya Stamina


 

Mkali wa Hip Hop kutoka Bongoland Stamina Shorwebwenzi ameachia albamu yake aliyoipa jina la Msanii Bora wa Hip Hop, kazi hii imetoka hivi karibuni na ni wazi imeenda kitaani na mashabiki na wapenzi wa muziki mzuri wameipokea kwa ukubwa sana.

 

Nondo za humo ndani ni za kutosha na ameshirikisha wakali wengi wa Bongo Flava ambao wameongeza ladha nzuri kwenye albamu yake. Nakusogezea nyimbo tano (5) kali kukusanua jumbe zilizomo na mengine ambayo unaweza kuyatarajia ukiwa unasikiliza albamu ya Stamina.

 

1.     Nioneshe featuring The Mafik.

 

Wimbo huu Una maudhuhi ya maombi kwa Muumbaji wetu na, humo ndani The Mafik wameimba kibwagizo (chorus) ambayo ni ya kugusa sana mistari yao inasema

“Mungu baba naomba unionyeshe njia, kabla uhai wangu hujauchukua, Baba nionyeshe, Mungu nionyeshe”

Kikubwa Stamina anamuomba Mungu kumuonesha njia ya kupita ili aweze kufanikiwa kwa faida ya watu wake wanaomtegemea. Ni wazi wimbo huu utawagusa wengi kwasababu ni maombi ya wengi wetu.


2.     Nakuja featuring Goodluck Gozbert.

 

Humu ndani Stamina amemshirikisha mmoja ya wasanii wakubwa na mkali wa muziki Injili Goodluck Gozbert. Kikubwa amezungumzia umuhimu wa kumtegemea Mungu kwa minajili ya kutaka kumtumikia yeye (Mungu) badala ya kuendelea kufanya dhambi na vitu ambavyo havimjengi. Stamina ameimba

“Na ile fimbo ya Musa ntaiomba kwa ruhusa yako niwachape wote hao wanovunja amri zako,

Naacha Whatsapp, naacha Twitter, naacha Tiktok, naacha Insta naacha vitu vyote nafungua page ya Kanisa. Naacha Snapchat,naacha udaku wote usio na maana, nakuja kwako kusoma maandiko yako Labana”.

 


3.     Wasaka Tonge featuring Ferooz.

 

Wimbo huu unazungumzia maisha halisi ya watu wenye hali ya chini ambao bado wanijtafuta kwa lengo la kufikia angalau hali nzuri ya kimaisha. Stamina ameshirikisha lijendi wa bongoflava Ferooz ambaye anajulikana kwa kuimba nyimbo za kugusa jamii, na kama kawaida haikuwa kazi mbovu kwasababu bado amewakilisha vyema, kibwagizo ama chorus imeimbwa nae Ferooz na ameimba;

“Mimi kuwa masikini hii yote mipango ya Mungu, leo nimekosa kesho nitapata riziki mafungu Mkiwaona waambieni ,waambieni jinsi tunavolia sisi wanyonge

Mkiwaona waambieni, waambieni maisha kwetu vita wasaka tonge”.

Ujumbe, mdundo na uimbaji wao ni wazi kuwa ni moja ya kazi bora kwenye albamu hii ya Msanii Bora wa Hip Hop.

 



 

4.     Tutaonana featuring Lily.

 

Jina lina wombo linasadifu ujumbe uliopo ndani kabla hata ya kusikiliza wimbo wenye, Tutaonana ni wimbo wa maombolezo na Faraja kwa wale waliondokewa na wapendwa wao. Stamina ameshirikisha mwanadada Lily ambaye sauti yake nzuri imefanya wimbo huu kuongeza mvuto ijapokuwa ni wa kuomboleza. Kibwagizo cha wimbo huu ni kibwagizo maarufu kwa maana hutumika sana kama wimbo wa kufariji wafiwa kuwa watakutana tena na wapendwa wao ikifika wakati.



 

5.     Kwa Ubaya featuring Linah.

 

Hili goma ni kwajili ya wale wenye maex ambao hawakuwa wema kwao, Stamina na Linah wamefanya kazi nzuri kufikisha ujumbe ambao kwa hakika unawagusa watu wengi. Ni Ni moja ya nyimbo nzuri kwenye albamu hii ya Msanii wa Hip Hop

Inaanza na sauti ya ndege mnana Linah akiimba;

“Hanogi kwa karafuu hanogi kwa chochote, si mkavu ni teketeke hsnifikishi mbigu ya saba hanitakatishu gugu gaga

Nilijua kibiriti kimejaa fumba fumbua ameolowesha mkaa, Haniridhishi ananitia kinyaa

Si mcheshi muda wote kazubaa ooh

Simsemi kwa ubaya aah, simteti kwa ubaya ooh,

Simsemi kwa ubaya aah, simteti kwa ubaya ooh”



 

Nimekuorodheshea chache tu kali kwenye albamu mpya ya Stamina, lakini itoshe kusema humo ndani ameua sana na kila wimbo unagusa maisha halisi ya watanzania na ni moja ya kazi bora kutokea kwa mwaka huu wa 2024. Chukua muda usikilize albamu hii kali halafu share hapo chini top 5 zako zilizopo kwenye Msanii Bora wa Hip Hop.

 

3 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page